Wednesday, July 1, 2015

KINANA AWAACHIA UJUMBE MZITO CCM UKEREWE

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kakukuru,Ukerewe ikiwa siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu amekamilisha ziara ya kutembelea majimbo yote ya Uchaguzi nchi nzima ambapo amejionea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi unavyooendelea pamoja na uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo akihutubia wakazi wa Kakukuru wilayani Ukerewe.
 Wakazi wa Kakukuru ,Ukerewe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuzindua shina la wakereketwa wa CCM Kakukuru.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa Kakukuru wilayani Ukerewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya mradi wa maji Kazilankanda uliopo kijiji cha Chabilungo ,Ukerewe utakaonufaisha vijiji 13 kutoka kwa msimamizi wa mradi Revocatus Migarambo .
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ukerewe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ukerewe ambapo aliwaambia wana CCM wasikae kimya badala yake waseme yale mambo ya wapinzani ambayo hayapo sawa, akitolea mfano halmashauri ya Ukerewe ipo chini ya upinzani na hakuna kinachofanyika hivyo si vyema kukalia jambo hilo ni vyema wananchi wafahamu .


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Nansio katika Uwanja cha Mongella ambapo aliwaambia wananchi hao wasichagueviongozi kishabiki kwani ushabiki unaweza wachelewesha sana kimaendeleo,alitoa mfano halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ipo upinzani na hakuna jambo la maendeleo linafanyika mpaka sasa.
 Bibi akisikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Mongella ,Nansio wilaya ya Ukerewe.
 Katibu Mkuu na ujumbe wake wakiondoka eneo la mkutano Nansio kwa mguu kwenda kupanda meli tayari kwa kurudi Mwanza mjini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliokuja kumpokea akitokea Ukerewe.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.