Sunday, June 28, 2015

KINANA ATIA FORA MWANZA MJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANONI UWANJA WA FURAHISHA, AWAPIGIA SALUTI

 Katibu  Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapigia saluti, maelfu ya wananchi, alipowasili kuhutubia  mkutano wake wa hadhara aliofanya leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwahamasisha maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo katika Vianja vya Furahisha Jijini Mwanza.
"'SAFI SANA"Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aonyesha dole gumba ambayo ni ishara ya CCM na kuonyesha kuwa mambo safi, alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Malikia wa taarab, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM, wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhmn Kinana uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Furahiha jijini Mwanza
 Mashabiki wakimg'amg'ania Khadija Kopa wakati akiimba wimbo maalum mbele ya mashabiki hao wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wake wa hadhara aliofanya katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
 Maelfu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
 Maelfu wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja hivyo leo.
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi y Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akitangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi y Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi yadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinna  baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
 Kinana akisindikizwa na maelfu ya wananchi alipokuwa akiingia kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo. Pmoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo n Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, akihutubia mkutano huo
Mmoja wa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, akiwa na mtoto wake aliyeshika kipeperushi cha CCM
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akihutubia kwenye mkutano huo
 Meya wa Jiji la Mwanza,  Stanslaus Mabula akihutubia kwenye mkutano huo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihitimisha kwa hotuba katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Furahisha jijini wanza leo. PIcha zote na Bashir Nkoromo na Adam Mzee
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.