Saturday, June 20, 2015

KINANA AING'ARISHA GEITA, LEO ASHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO, MIKUTANO YAKE YA HADHARA YAZIDI KUFURIKA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo.
 Melfu ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowahutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimhoji Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya maji mkoani Geita, (Gewasa), Clemence Chagu, kuhusu utekelezwaji wa mradi wa maji katika jimbo la Geita, alipohutubia mkutamo wa hadhara akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na uhai wa Chama katika mkoa wa Geita leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika leo, mjini Geita.
 Mbunge wa jimbo la Busanda Lorencia Bukwimba akihutubia katika mkutano huo
 Mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano huo akipiga mbinje baada ya kuvutiwa na maneno ya Kinana katika mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionyesha alama ya dole kuonyesha kuwa mambo yameenda vizuri wakati akiondoka baada ya kuhutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kalangalala mkoani Geita

KABLA YA MKUTANO WA HADHARA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda kwenda juu kupiga misumari kwenye kenchi aliposhiriki uwekaji kenchi kwenye Nyumba ya Mganga inayojengwa katika zahanati ya Kijiji Nyanguku, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga msumari kwenye kenchi aliposhiriki ujenzi wa nyumba hiyo ya mganga, leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushiriki upigaji kenchi kwenye nyumba ya mganga inayojengwa katika kijiji cha Nyankungu, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Napa Nnauye na Mkurugenzi wa Mawasiliano Makao makuu ya CCM, Godfrey Chongolo wakiwatazama mafundi waliokuwa wakipiga lipu jengo la shule ya sekondari ya Ihanamilo, mkoani Geita,  kabla ya Katibu Mkuu wa CCM kushiriki upigaji ripu huo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki upigaji lipu kwenye jengo hilo la shule ya sekondari Inahamilo, leo
 Watoto wenye kipaji cha aina yake, wakitoa mashairi ya kukisifia Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipofika shule ya sekondari ya Inahamilo kukagua ujenzi wa vymba vitatu vya maabara katika shul ya Ihanamilo mkoani Geita leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ugeni wake wakiwasilikiza watoto hao
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwa amewabeba watoto hao baada ya kumfurahisha
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia, Mary Kasanga, alipokagua shughuli za wachimbaji dhahabu wadogo wadogo, katika Kijiji cha Mgusu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji waIlani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsaidia kuponda mawe, Mary Kasanga, alipokagua shughuli za wachimbaji dhahabu wadogo wadogo, katika Kijiji cha Mgusu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji waIlani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita.
 Katibu Mkuu a CCM Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi ya kulainisha udongo kwa kuunguza kwa moto kabla ya kuuchambua dhahabu, lipokagua shughuli za wachimbaji dhahabu wadogo wadogo, katika Kijiji cha Mgusu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji waIlani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita.
 Katibu Mkuu akitazama mitambo ya kuchakata mchanga alipotembelea wachimbaji hao wadogowadogo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiendelea kutazama shughuli za wachimbaji hao
 Kinana akiendelea kuangalia shughuli za wachimbaji hao
 Katibu Mkuu wa CM Abdulrahman Kinana akionyeshwa dhahabu iliyopatikana

 Kijana akiwa katika kazi ya kusafisha dhahabu aliyopata
 Wakazi wa Kijiji hicho cha wachimbaji wadogo wakimshangilia Kinana alipozungumza nao baada ya kukagua shughuli zao
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha wachimbaji dhahabu wadogo wadogo
 Mbunge wa Busanda Lorencia Bukwimba akisalimia wananchi katika mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya katika kijiji hicho cha wachimbaji wadogo wa dhahabu
 Wananchi wakiwa wamekaa
 akipaka rangi
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akicharaza kinanda baada ya msafara wa Katibu Mkuuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwasili katika Kata ya Kasota, kukaga mradi wa umeme Vijijini (REA) akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta waya wa umeme, wakati wa kutandaza nyanya za umeme kwenye mradi wa umeme Vijijini (REA) katika Kata ya Kasota mkoani Geita
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua Ofisi ya CCM Kata ya Nzera, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhi wa Chama mkoani Geita leo.
Katibu Mkuu waCCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Kata ya Nzera, mkoani Geita, baada ya kufungua Ofisi ya CCM ya Kata hiyo, leo. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CC, Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mtaro wa bomba la maji katika Kata ya Kalangalala, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita leo
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Geita,wakati Kinana alipozungumza nao akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo la Geita.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwaandaa wajumbe, Kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza nao katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani Geita. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.