Saturday, May 23, 2015

KAMATI KUU YAISHAURI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA SERIKALI KUZUNGUMZA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti leo kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma, tarehe 23 Mei 2015.
                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu katika kikao chake cha tarehe 22/05/2015 mjini Dodoma pamoja na mambo mengine imepokea na kutafakari kwa kina taarifa ya maandalizi ya mchakato wa kupiga kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa.

Baada ya kutafakari na kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika maandalizi hayo, Kamati Kuu ya CCM inaishauri serikali kwa kushauriana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakizingatia changamoto zilizopo na hali halisi ya mchakato huu, kutafuta njia muafaka ya kulishughulikia na kulihitimisha jambo hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM (T).
23/05/2015
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.