Thursday, March 12, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA DODOMA LEO

  • Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo amemaliza ziara yake ya siku 9 katika mkoa wa Dodoma ambapo amesafiri wastani wa kilometa 2289, ametembelea wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi.
  • Amehutubia jumla ya mikutano 90 ikiwa pamoja na mikutano ya hadhara  81 na mikutano ya ndani 9.
  • Ameshiriki ,Amekagua,amezindua na kuweka mawe ya msingi  katika jumla ya miradi 73 ikiwemo miradi ya Chama 11 na miradi ya maendeleo ya wananchi 62.
  • Amepokea wanachama wapya wa CCM 8245 wakiwemo 44 kutoka vyama vya upinzani.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Ikengwa ambacho wananchi wake wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina yao na hifadhi ya Taifa ya Mkungunelo.
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa Zabein Mhita akipiga magoti kama ishara ya kuomba kwa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Ikengwa wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma.
 Wazee wa kijiji cha Ikengwa wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao.
 Maganda ya risasi amabayo wananchi wa kijiji cha Ikengwa waliyaokota , wananchi hao wamekuwa wakilalamika kupigwa risasi na askari wa wanyama pori.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo Alhaji Omar Kariati akisoma risala yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kwadelo ambapo alisema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi umekamilika kwa asilimia 100 katika Kata yake.
 Wananchi wa kata ya Kwadelo wakinyoosha mikono juu kuonyesha ishara ya kukubaliana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kwadelo.
 Katibu Mkuu wa CCM akisoma jiwe la msingi baada ya kufungua ofisi ya kata CCM Kwadelo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wakazi wa kijiji cha Mnenia
 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Shaban Kisu akisalimia wananchi wa Kondoa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa Kondoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba ,Kondoa mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akiwahutubia wakazi wa Kondoa na kuwaambia wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali na ofisi yake haitokata jina la mtu aliyependekezwa na wananchi.
 Wananchi wa Kondoa wakisikiliza kwa makini mkutano wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kondoa na kuwaambia muda wa kujiandikisha kupiga kura ukifika wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata yaki yao ya msingi ya uhalali wa kupiga kura.


Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.