Thursday, January 15, 2015

ZIARA YA WAZIRI NYALANDU MJINI RIADHI WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akiwa katika mazungumzo na Mwana Mfalme wa Saudia, Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, kuhusiana na masuala ya uhifadhi, mjini Riyadhi, jana.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akiwa katika mazungumzo na Mwana Mfalme wa Saudia, Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, kuhusiana na masuala ya uhifadhi, mjini Riyadhi, jana. Wengine ni ujumbe uliofuatana na Lembeli, ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk. Adelhem Meru, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi Arabia jijini Riyadh, Saudi Arabia.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Adelhem Meru (katikati), akizungumza kwenye mkutano baina ya ujumbe wa Tanzania na Saudi Arabia. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Profesa Abdillah Omari.
 UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakiwa kwenye picha ya pamoja na zawadi waliyopewa na Mwana Mfalme Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia, Profesa Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Herman Keraryo.


 Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia, akizungumza wakati wa mkutano huo. Pembeni ni Waziri Nyalandu.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.