Wednesday, January 21, 2015

ZIARA YA KINANA KUSINI UNGUJA ILIVYOFANA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Dunga mara baada ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya wilaya.Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia samaki aina ya Taa kwenye soko la samaki Unguja Ukuu jimbo la Koani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wauza samaki wa soko la samaki huko Unguja Ukuu jimbo la Koani.
 Mwakilishi wa jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Gavu akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kueleza mipango mbali mbali iliyofanywa na inayoendelea kufanywa kwa ajili ya kuisaidia jamii na maendeleo kwa jumla katika Jimbo la Chwaka.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutika mbegu (kupanda) za karafuu kwenye shamba la viungo na matunda Kwambani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mzee Salim Suleiman wa maskani ya Moto,Miwani Zanzibar, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdala Ali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Machui ,Unguja ya Kusini mara baada ya kutembelea mradi wa maji utakaowafaidisha wananchi wa Machui na kuwaambia wananchi wanapaswa kutambua juhudi za serikali katika kuleta maendeleo hivyo ni jukumu lao kulinda miradi yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu kwenye viwanja vya mikutano Tunduni, kijiji cha Tunduni jimbo la Uzini wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
 Wananchi wakiwa wamehudhuria kwa wingi mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM jimbo la Uzini Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Mheshimiwa Vuai Ali Vuai akiwahutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Tunduni ,wilaya ya kati mkoa wa Kusini Unguja.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdala Ali akitoa salaam kwa wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara Tunduni.
 Mbunge wa Jimbo la Uzini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa
Mohamed Seif Khatib Dk.Mohamed Seif Khatibu akihutubia wananchi waliofika kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara Tunduni.
 Wananchi wakiashiria kukubali hoja mbali mbali zilizotolewa na viongozi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi jezi kwa Hamisi Amour Hamisi Katibu wa timu ya mpira wa miguu FC Morocco almaarufu kwa jina la Bambi,zaidi ya timu 38 za jimbo la uzini zilipewa jezi na mipira kutoka kwa Mbunge wao Dk.Mohamed Seif Khatibu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tunduni mkoa wa Kusini Unguja na kuwaambia huu ni wakati wa kuielewa vizuri Katiba iliyopendekezwa kwani imeweka wazi masuala yote yanayohitajika na Wazanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambako aliwaambia Viongozi wa CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi na CCM haitokuwa tayari kuona viongozi wanakivuruga chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Tunduni, jimbo la Uzini Zanzibar.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi kutoka upinzani zilizorudishwa na Bi.Fatma Kassim aliyeamua kujiunga na CCM yeye pamoja na ndugu zake watano.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiinua mkono juu kama ishara ya kula kiapo wakati wa kuwaapisha wanachama wapya zaidi ya 400 waliojiunga na CCM jimbo la Uzini Zanzibar, wengine kwenye picha ni Katibu wa CCM mkoa wa Kusini Unguja Sauda Mpambalyoto,Mbunge wa jimbo la Uzini Dk.Mohamed Seif Khatibu,Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Unguja  Ramadhani Abdala Ali.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.