LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 10, 2015

TANZANIA YAOMBOLEZA NA UFARANSA

 Mwakilishi wa Kudumu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako  Manongi, jana Ijumaa alijumuika na wawakilishi wa  Kudumu wa Mataifa mengine  katika Umoja wa Mataifa,  waliojitokeza katika kile kinachoweza kuelezwa kama mshikamano kusaini  kitabu cha  Maombelezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Ufarasa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio linaloelezwa kuwa  la kigaidi lililotokea siku ya  Jumatano
ambapo  watu  kumi na mbali wakiwamo waandishi wa  gazeti la  Charlie Hebdo walipoteza maisha katika shambulio hilo. 

Pichani, Balozi Tuvako  Manongi akibadilishana   mawazo  na Mabalozi  wenzie  muda mfupi kabla ya  kusaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio la jumatano  ambapo watu  kumi na mbili wakiwamowaandishi wa gazeti la Charlie  Hebdo  walipoteza maisha
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiandika  salamu za rambirambi kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi ambapo watu kumi na  mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo waliuawa

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages