LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2015

MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
 Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.

Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.

Dotto Mwaibale

JAJI Mkuu Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika ngazi husika pindi  wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo wake.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.

"Katika rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani au sehemu husika na sheria itafuatwa," alisema Jaji Chande.

Kadhalika, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi zote.

Mwenyekiti wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.

"Mahakama imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio  kufanyika ndani ya jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono imetawala katika sekta mbalimbali," alisema Kileo.


Lakini kwa sasa  chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages