Thursday, January 15, 2015

KINANA : CCM ITASHINDA ZANZIBAR


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi Wilaya ya Amani,Zanzibar ambapo aliwaambia CCM imejipanga vizuri kuhakikisha inashinda kwenye chaguzi zinazokuja Zanzibar kwani ndio Chama pekee chenye sera nzuri taratibu na muundo unaoeleweka.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubiawananchi wa Wilaya ya Amani na kuwaambia kuwa Katiba iliyopendekezwa ni moja ya Katiba bora kwani imezingatia masuala yote muhimu ambayo Zanzibar ilihitaji yawepo kwenye Katiba hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Amani kwenye uwanja wa mikutano kwa Binti Imrani ambapo aliwaeleza wananchi hao ziara zake zimelenga mambo makuu wawili kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 na kukagua uhai wa Chama .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwa kwenye viwanja vya Binti Amrani, wilaya ya Amani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Mhe,Borafya Silima Juma akihutubia umati uliofika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye yupo ziarani kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Amani Zanzibar ambapo alitoa pongezi za Kamati Kuu kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (ZNZ) Dk.Ali Mohamed Shein kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa ziara yake ya kichama Zanzibar.:

 Wananchi wakionyesha ishara ya kukubaliana na sera za viongozi wao.
 Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Amani kwenye viwanja vya Binti Amran ambapo aliwataka wananchi hao kutohadaika na maneno ya wapinzani ambao hawaitakii mema Zanzibar.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
 Kila mtu huguswa na jambo lake awapo uwanjani kwenye mikutano ya CCM
Viongozi wakiwa wamekaa chini pamoja na wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Binti Amran ,Mpendae Zanzibar.
Mbunge wa jimbo la Mpendae CCM Salim Hassan Abdullah Turky almaaruf kama Mr.White akiwa wamekaa chini pamoja na viongozi wengine wa chama na kiserikali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye viwanja vya Binti Amran ,Zanzibar.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.