Wednesday, January 14, 2015

KINANA AWAPONGEZA VIONGOZI WA CCM ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI VIZURI

  •  Ashiriki shughuli mbali mbali za kijamii
  • Atembelea majimbo matano ( 5 ) ya wilaya ya Mjini Zanzibar
  • Awataka Viongozi kuwajali vijana ,kuwasaidia katika masuala mbali mbali ya msingi
  • Awaambia wananchi Katiba inayokuja imezingatia mahitaji ya Zanzibar
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia vijana wapatao 500 wa Kituo cha Vijana ( Tanzania Youth Icon) cha Kuwaendeleza na Kuwawezesha katika masuala mbali mbali kama Elimu, Kujiajiri na Michezo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati)akijaribu kutengeneza mapambo yatokanayo na karatasi kwa msaada wa mwalimu Abdala Suleiman (kushoto) wa Kituo cha Vijana ( Tanzania Youth Icon) cha Kuwaendeleza na Kuwawezesha katika masuala mbali mbali kama Elimu, Kujiajiri na Michezo kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kikwajuni mheshimiwa Hamad Masauni Yussuf.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wa CCM na wananchi kutandaza bomba la maji safi na salama katika eneo la Shehia ya Kilimani wilaya ya Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kupika na vijana wa Kituo cha Vijana ( Tanzania Youth Icon) cha Kuwaendeleza na Kuwawezesha katika masuala mbali mbali kama Elimu, Kujiajiri na Michezo kilichopo Muembe Madema Zanzibar.
 Vijana wa CCM wilaya ya Mjini wakifanya michezo ya kujirusha kumfurahia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyetembelea Kituo cha Vijana ( Tanzania Youth Icon) cha Kuwaendeleza na Kuwawezesha katika masuala mbali mbali kama Elimu, Kujiajiri na Michezo
 Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana ( Tanzania Youth Icon) cha Kuwaendeleza na Kuwawezesha katika masuala mbali mbali kama Elimu, Kujiajiri na Michezo akionyesha jezi alizokabidhiwa kwa ajili ya timu ya mpira wa kikapu.

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye maeneo ya Mikunguni jimbo la Kwahani ambapo alizindua mradi wa maji.
 Watoto wakichezea maji baada ya kuzinduliwa kwenye jimbo la Rahaleo
       Balozi Ali Karume akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili  Miembeni jimbo la Kikwajuni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili Vikokotoni jimbo la Mji Mkongwe ambapo alishiriki kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa kitega uchumi cha Tawi la CCM Vikokotoni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchapia udongo kwenye madirisha ya ofisi ya Chama Mwembeladu katika jimbo la Raha Leo,Zanzibar.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.