Sunday, January 18, 2015

KINANA AWAJENGEA UWEZO WANA CCM MKOA WA MAGHARIBI WAAHIDI KUSIMAMA IMARA

  • Zaidi ya wanachama 1000 wajiunga na CCM mkoa wa Magharibi
  • Hotuba zake na zawa gumzo mjini
  • Asisitiza mshikamano kwa wanachama wa CCM

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha wakishiriki kujenga ofisi ya Tawi la CCM Bububu,jimbo la Bububu wilaya ya Mfenesini.

 Mwakilishi wa Jimbo la Dole ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Shawana Buheti Hassan akitoa salaam za pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa  kufanya ziara nchi nzima ya kujenga na kuimarisha chama.
 Kaibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Dole Silvester Mabumba kwa kukabidhi Ambulance itakayosaidia wananchi wa Jimbo la Dole.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza bomba la maji Wadi ya Mbuzini jimbo la Mfenesini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji kama kuzindua rasmi huduma ya maji salama wadi ya Mbuzini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia zao la Vanilla kwenye shamba la Viungo Mwakaje.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangaliaviungo vinavyouzwa na wanakikundi cha Mwakaje huku akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi Ndugu Othman Abdulrahman Mohamed.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mti wa mdalasini kwenye shamba la viungo la kikundi cha Mwakaje.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda bilinganya kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Magharibi Yusuph Mohamed Yusuph (katikati) na Naibu Katibu Mkuu CCM ( Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
 Naibu Katibu Mkuu CCM ( Zanzibar) Vuai Ali Vuai akitoa maelezo mafupi juu ya historia ya kilimo cha Viungo Zanzibar kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shamba la viungo (spices) Mwakaje.
 Katbu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakina mama wa kikundi cha kijasiriamali cha Mwenye Kusubiri Hachoki wa Mtopepo ,Zanzibar.
 Katbu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimzawadia mtoto Hawana Othman (8) anayesoma darasa la kwanza Skuli ys Chumbuni gauni lililotengenezwa  na wakina mama wa kikundi cha kijasiriamali cha Mwenye Kusubiri Hachoki wa Mtopepo ,Zanzibar.
 Vijana wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwageji wilaya ya Mfenesini,
 Waziri Kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wakazi wa Mfenesini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kwageji .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mfenesini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kwageji ambapo aliwaambia wananchi hao wapinzani hawajielewi kiasi cha kukingana na kauli zao zilizotolewa mpaka kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
 Wananchi wakishangilia hotuba za viongozi wao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwageji,wilaya ya Mfenesini.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) akihutubia wakazi wa Mfenesini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwageji.
 .
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Magharibi Yusuph Mohamed Yusuph akihutubia wakazi wa mfenesini na kuwaambia wananchi hao CCM ya sasa haitokubali kuonewa kwa namna yeyote vile.
 Wananchi wa Mfenesini Zanzibar wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasalimu wananchi hao na kuwashukuru kwa ushirikiano mzuri ,Kinana aliwasisitiza wana CCM kushikaman na kuwa kitu kimoja .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa Mfenesini kwenye uwanja wa Kwageji ambapo alihimiza wana CCM kushikamana kuwa wamoja na kuwa waadilifu.
 Wanachama wapya wakila kiapo,zaidi ya wanachama 1000 wamejiunga na CCM katika mkoa wa Magharibi.

Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.