Tuesday, December 16, 2014

KONGAMANO LA KUJADILI JAMII ZA KIASILI (INDIGENOUS PEOPLE) LAFUNGULIWA DAR


001
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akitoa hotuba yake wakati akifungua kongamano la siku mbili la bara la Afrika la kujadili masuala ya jamii za kiasili (indigenous people) lililofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
Kongamano hilo linajadili changamoto zinazowakabili watu wa jamii za asili na namna ya kuboresha maisha ya jamii hizo bila kupoteza uasilia wao huku mada kuu ikiwa ni suala la mifumo ya upatikanaji wa chakula chao na maisha endelevu. Mapendekezo ya kongamano hilo yatawasilishwa katika mkutano wa dunia wa kujadili masuala ya jamii za kiasili utakaofanyika mjini Roma Italia, februari mwaka 2015.
Katika hotuba yake Waziri Kamani amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa kuandaa sera mahsusi inayotambua uwepo wa jamii hizo, utamaduni na desturi za jamii za kiasili kama nyenzo ya kuzisaidia jamii hizo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
002
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw.Francisco Pichon akieleza namna shirika lake linavyotoa kipaumbele katika kushughulikia masuala yanayohusu jamii za asili na hivyo kuitaka serikali na wadau kufanya kazi kwa pamoja katika kushughulikia masuala hayo ili kupata matokeo yanayokusudiwa.
Waziri Kamani pia ameipongeza IFAD kwa kuanzisha mfuko maalum wa miradi ya jamii za asili unaosimamiwa na watu wa jamii za asili wenyewe. mpaka sasa mfuko huo umeshafadhili miradi midogo midogo 100. IFAD pia imeanzisha jukwaa mahsusi la mijadala kuhusu haki na nafasi za watu wa jamii ya kiasili kwa kuzingatia azimio la Umoja wa Mataifa la haki za watu wa jamii ya kiasili.
Waziri Kamani alisema zerikali ya Tanzania inazitambua jamii za asili ikiwamo wahadzabe, wasandawi na masai na kusema serikali itashirikiana na wadau katika kuzilinda jamii hizo na kuzikabili changamoto wanazokumbana nazo ili kuboresha maisha yao.
003
Wadau mbalimbali kutoka Nchi za afrika wakiwa kwenye kongamano hilo ambalo pamoja na mambo mengine linajadili namna ya kuzisaidia jamii za asili kuwa na maisha endelevu bila kuharibu mazingira yao.
004
005
006
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.