HABARI MPYA

Your Ad Spot

Dec 22, 2014

KIKWETE AHUTUBIA TAIFA KUPITIA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Saidi Mecki Sadiki akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za Sekondari mjini Dar es Salaam pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.(Picha na Adam Mzee)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.( Picha na Adam Mzee
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)
 Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
 Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
 Ukumbi wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Ukumbi ulifurika kila kona.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Wananchi wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages