Saturday, October 11, 2014

KINANA AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE MKOA WA IRINGA

*AANZA ASUBUHI KWA KAZI KIBAO
*MAELFU WAFURIKA KATIKA MKUTANO WAKE IRINGA MJINI
*MAKATIBU WATATU CHADEMA WAHAMIA CCM
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, leo Oktoba 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Iringa
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emmanuel Ngaladi baada ya kupokea kadi yake ya Chadema, hatua iliyofuatiwa na kutangaza kwake kuhamia CCM katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo
 Katibu wa Chadema, jimbo la Mufindi Kusini akitangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo, Mwembetogwa, Iringa mjini. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyempandisha jukwaani kutangaza uamuzi huo
Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi kutoka kwa Katibu Mwenezi wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Sebastiab Koloa, Tanga, Mdillah  Osward ya kutangaza  kuhamia CCM katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo
Katibu Mwenezi wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Sebastiab Koloa, Tanga, Mdillah  Osward, akitangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo, Mwembetogwa, Iringa mjini. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyempandisha jukwaani kutangaza uamuzi huo
 Kada machachari na msomi wa Chadema Gerald John akitangaza kukihama chama hicho katika mkutano huo wa Mwembetogwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasluti wananchi waliokuwa wakimshangilia alipowasili kwenye Viwanja vya Mwembetogwa, kuhutubia mkutano huo wa hadhara Iringa mjini
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mwembetogwa akitokea hospitali kupata matibabu baada ya kuumia mkono wakati akicheza mpira leo asubuhi
 Wananchi wakitoa ujumbe kupitia mabango kwenye mkutano huo wa Mwembetogwa mjini Iringa leo
 Vijana Chipukizi wa CCM, wakienda kwa ukakamavu kwenye mkutano huo wa hadhara wa Kinana uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo.
Baadhi ya viongozi na maofisa wa CCM wakishiriki na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kula chakula cha mchana kwa Mamalishe mjini Iringa leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanjavya Mwembetogwa leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila chakula cha mchana kwa Mamalishe, mjini Iringa leo, kabla ya kwenda kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu
 Mamalishe akimnawisha Kinana baada ya kula
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la madereva wa daladala, wakereketwa wa CCM  Iringa mjini kabla ya kwenda kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa SACCOS ya Masoko Vicoba, mjini Iringa leo
Wanachama wa Saccos hiyo wakimsikiliza Kinana
 Kinana akiwasalimia wanachama wa Saccos hiyo alipoingia ukumbini kuzungumza nao mjini Iringa leo asubuhi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kabla ya kuingia kwenye mkutano wa Wana-Saccos hao mjini Iringa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wa CCM eneo la Kihesa  Mwang'ingo leo asubuhi
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wazee, alipotembelea shina namba moja la Lucas Mkazizi eneo la Mkimbizi, Iringa Mjini leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisalimia kinamama
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maji Mjumbe wa Shina namba moja, Lucas Mkazizi, wakati yeye na msafara wake walipokunywa chai ya asubuhi nyumbani kwa mjumbe huo baada ya kikao cha shina hilo
 Kinana akinywa chai nyumbani kwa balozi huyo, mtaa wa Mkimbizi, Iringa mjini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaslimia watoto wa kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Upendo Centre, waliofika kumlaki kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini leo asubuhi
 Watoto wakiwa katika mapokezi hayo ya Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini leo asubuhi. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.