LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO KATI YA VYOMBO VYA HABARI NA VYOMBO VYA ULINZI, USALAMA NA SHERIA, JIJINI DAR ES SALAAM.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa Mashauriano kati ya Vyombo vya Habari na Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2014. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) Picha na OMR

  Rais wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Jaji Thomas Mihayo, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo,  uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi Mukajanga, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo,  uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
  Baadhi ya Washiriki, waandishi wa habari na Wahariri wa habari kutoka Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi mkutano huo leo.  Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, baada ya kufungua mkutano huo. Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi  Mukajanga, wakati akiondoka mara baada ya kufungua mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Asah Mwambene. Picha na OMR


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages