LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2024

TANROADS YAANIKA MAFANIKIO MIAKA MITATU YA RAIS DK. SAMIA, YAKUNA KICHWA KUJENGA MIUNDOMBINU ITAKAYOHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

Na Bashir Nkoromo, CCM's Official Blog, Dar
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imesema, inakuna vichwa kuona namna inatakvyoweza kujenga miundombinu inayohimili uharibifu ambao husababishwa na mvua kama za El-Nino, Kimbunga Hidaya na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Ephata Mlazi, wakati akiwasilisha mafanikio ya Wakala hiyo katika miaka mitatu ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, kwenye Kikaokazi chake na Wahariri na Waandishi wa habari, kilichofanyika chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 26, 2024.

Amesema Wakala imepokea fedha nyingi za Serikalo kwa ajioi ya kufanyakazi kubwa katika kurejesha hali ya miundombinu iliyoharibiwa na adha iliyopita ya Mvua za El-Nino na Kimbunga Hidaya.

Akieleza mafanikio katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, Mhandisi Mlavi amesema TANROADS ambayo inasimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya kilometa 37,225.71, jumla ya Kilometa 15,343.88 zimekuwa kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Amesema Kilometa 1,198.50 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, Kilometa 2,031.11 ziko kwenye hatua za ujenzi kwa kiwango cha lami na jumla ya Kilometa 2,052.94 na Madaraja mawili (2) yamefanyiwa Upembuzi Yakinifu tayari kujengwa kwa kiwango cha Lami.

Mhandisi Mlavi amesema, jumla ya Kilometa 4,734.43 na Madaraja 10 yapo kwenye hatua ya Upembuzi Yakinifu na Miradi ya Barabara yenye urefu wa Kilometa 5,326.90 na Madaraja saba (7) ipo kwenye hatua ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina ikiwa ni maandalizi ya kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aliainisha madaraja yaliyojengwa kuwa ni tisa (9) ambayo aliyaja kuwa ni Gerezani – Dar es Salaam, Tanzanite – Dar es Salaam, Wami – Pwani, Kitengule - Kagera, Kiyegeya – Morogoro, Ruaha – Morogoro, Ruhuhu - Ruvuma, Mpwapwa - Dodoma na Msingi - Singida na kutaja matano (5) yanayojegwa kuwa ni Pangani – Tanga, J.P. Magufuli – Mwanza, Lower Mpiji – Dar es Salaam, Mbambe – Pwani na
Simiyu – Mwanza.

Kuhusu kusimikwa taa za barabarani, Mhandisi Mlavi amesema, Wakala imepokea fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kusimika taa za baraarani nchini kote na kutaja mikoa ambayo tayari imekwisha simikwa taa hizo kwenye baadhi ya Barabara zake kuwa ni Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Geita, Iriinga, Kagera, Kigoma, Kilimajaro, Lindi, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida, Songwe, Tabora na Tanga.

Upande wa Wakandarasi wa ndani, amesema TANROAS inajikita katika kujenga Uwezo wa Makandarasi Wazawa, kutenga asilimia kumi (10) ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa ajili ya Miradi ya mafunzo kwa vitendo, kutenga angalau asilimia thelathini (30) ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa wazawa.
 
Kuhusu makundi maalum, amesema, halikadhalika, TANROADS inajikita katika kutenga angalau asilimia tano (5) ya bajeti ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya makundi maalum bila kuacha ushiriki wa wanafunzi na wahitimu katika miradi, na kazi za matengenezo ya barabara na madaraja zitekelezwe na Makandarasi Wazawa na kusimamiwa na Washauri Elekezi Wazawa tu.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Ephata Mlazi, akiwasilisha mafanikio ya Wakala hiyo katika miaka mitatu ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, kwenye Kikaokazi chake na Wahariri na Waandishi wa habari, kilichofanyika chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 26, 2024.

Afisa Habari Ofisi ya Msajili wa Hazina Alex Malanga, akiendesha Kikaokazi hicho baina ya Uongozi wa TANROANDS na Wahariri na Waandishi wa Habari, kilichofanyika kwa Uratibu wa Ofisi hiyo, jijini Dar es Salaam, leo.
Meneja Mawasiliano wa TANROADS akimwalika kuzungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Ephata Mlazi akizungumza.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi John Mkumbo na Mhandisi Clever Akilimali (kulia) pia wa TANROADS mkoa huo, wakiwa kwenye kikaokazi hicho.
Wahariri wakongwe Mzee Joe Nakajumo na Mzee Yasin Sadiki wakiwaa kwenye kikaokazi hicho.
Viongozi wa TANROADS wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahariri wa Habari mwishoni mwa kikaokazi hicho.

Tafadhali pitia Wasilisho kama lilivyosomwa na Mhandishi Mlavi👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages