LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 27, 2024

KIKWETE AKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MJINI MWANZA.

 - Akutana na makundi mbalimbali kuhamasisha shamra hizo

-Awatembelea Vijana wa Halaiki.


Waziri wa Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mh. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza ikiwa ni kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotaraji kuhitimishwa mkoani hapo Tarehe 14 Oktoba, 2024 katika uwanja wa CCM kirumba jijini hapo. 


Akiwa mjini Mwanza ,Waziri Kikwete amepata nafasi ya kukutana na makundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa kilele hicho na wiki ya Vijana ambayo inataraji kuanza tarehe 8 hadi 13 Oktoba 2024 katika viwanja vya furahisha. Waziri Kikwete ambaye alikuwatana na makundi ya Vijana Wasanii katika fani mbalimbali na baadae kukutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Walimu wa sekondari na vyuo toka wilaya zote za Mkoa huo, alitumia nafasi hiyo kuwahimiza kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha kuwa wanaulaki Mwenge kwa shamra nyingi na kushiriki kilele cha wiki ya vijana. 


Baada ya mikutano hiyo ya Wadau , Waziri Kikwete alifika Uwanja wa CCM Kirumba kuona maandalizi ya haraiki ambapo alishuhudia vijana wakiendelea na maandalizi yao na katika salamu zake aliwapongeza walimu wa vijana hao na kuwatia moyo wanafunzi ambao wameandaliwa vizuri. Uwanjani hapo 

 

Waziri wa Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mh. Ridhiwani Kikwete  akikagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotaraji kuhitimishwa mkoani hapo Tarehe 14 Oktoba, 2024 katika uwanja wa CCM kirumba jijini hapo. 

Ridhiwani akijadiliana jambo na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wa Mwanza.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages