MKOA wa Pwani jana umefanya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata tatu za Fukayosi iliyoko Wilaya ya Bagamoyo, Kata ya Mlanzi iliyoko Wilaya ya Kibiti na Kata ya Msangani iliyoko Wilaya ya Kibaha Mjini huku ikiwaacha midomo wazi Vyama Pinzani vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi katika Kata ya Msangani ni ADA - TADEA, CCK, DEMOKRASIA MAKINI, DP, N.R.A, UMD na UPDP. Katika Kata ya Mlanzi Vyama vilivyoshiriki ni ACT - WAZALENDO, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, N.R.A, UDP, UMD na UPDP. Katika Kata ya Fukayosi ni CCK, DEMOKRASIA MAKINI, UDP na UMD.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani ndg David Mramba, wagombea wa CCM walioshinda ni Ndg. Mrisho Saidi Some wa Kata ya Fukayosi Wilaya ya Bagamoyo aliyepata kura 5883 Kati ya kura halali 5960 sawa na asilimia 98.7. Mwingine ni dg. Athumani Ally Mketo wa Kata ya Mlanzi Wilaya ya Kibiti kura 1592 Kati ya kura halali 1732 sawa na asilimia 91.9.
Huku Ndg. Yohana Gunze wa Kata ya Msangani Wilaya ya Kibaha Mjini amepata Kura 5862 Kati ya kura halali 5909 sawa na asilimia 99.20. Wana CCM wamewapongeza viongozi wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini kwa mipango mizuri iliyosababisha Kata ya Msangani iliyoko chini ya wilaya hiyo kumfanya mgombea wake kushinda kwa kishindo na kuongoza kimkoa kwa kushinda kwa kura nyingi. Wamepongeza pia viongozi wa CCM kata ya Msangani na wana CCM wote wakiwamo viongtozi na wajumbe wa kamati za ushindi na wana CCM kwa ujumla kufanikisha ushindi huu mkubwa.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇