Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amewataka wazazi kuacha tabia ya kukimbilia kuwaozesha mabinti zao kabla hawajapata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea.
"Tusiwakimbize mabinti kwenda kuolewa kabla hawajapata ujuzi, wakienda kuolewa wakiwa na ujuzi, tunakuwa tumewasaidia kuwa imara, kujitegemea, kujisimamia, lakini pia kuimarisha ndoa zao huko wanapokwenda.
Tukiwapeleka kuolewa kabla ya kujifunza ufundi, tutakuwa tumewatengenezea mazingira magumu huko kwenye ndoa zao, watakuwa wategemezi kwa kila kitu." Katibu Mkuu Chongolo akasema, katika mikutano ya Mashina Kilindi mkoani Tanga, jana, Juni 2, 2021. Tafadhali msikilize, Bofya Hapo👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇