Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage
akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu
mafanikio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya
Kwanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Nec, Dk. Wilson Charles Mahera.
Na Richard Mwaikenda
TUME ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), imeanisha njia tatu za Mpiga Kura kumwezesha kuhakiki kirahisi taarifa
zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Awamu ya Pili katika zoezi
linalotarajiwa kuanza Aprili 17 mwaka huu.
Njia hizo ni; kuhakiki
taarifa zao katika orodha itakayokuwa imebandikwa katika vituo,kutumia mfumo wa
Voters’ Interaction Systems (VIS),
ambapo Mpiga kura kupitia simu yake ya kiganjani atapiga namba *152*00# na kufuata maelekezo. Huduma hii ni ya bure.
Vilevile, kwa kupitia Tovuti ya Tume (_HYPERLINK "http://www.nec.go.tz"_www.nec.go.tz_),atahakiki
taarifa zake katika sehemu iliyoandikwa “uhakiki” na kuendelea kufuata
maelekezo.
Pia, Wapiga Kura watahakiki kupitia kituo cha Huduma kwa
Wapiga Kura (Call centre) ambapo wananchi watapiga simu bure kupitia namba ya
simu ya kituo ambayo ni 0800782100 na kupata usaidizi katika kuhakiki taarifa
zao.
Njia hizo zilitajwa na
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu,Semistocles
Kaijage wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa kuwapa
taarifa kuhusu mafanikio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Awamu ya Kwanza, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaijage alisema kuwa,Tume imeweka
njia zote hizo ili iwe rahisi kwa Wapiga Kura wote kuhakiki taarifa zao.
Alisema kuwa,Daftari la
Awali litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha Wapiga Kura
katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza, lakini
uboreshaji wa Daftari wa Awamu ya Pili na uwekaji wa Pingamizi utafanyika
katika vituo vilivyoteuliwa na Tume katika kila Kata.
Idadi ya Vituo hivyo nchi
nzima ni Elfu nane na thelathini na moja
(8031).
"Katika vituo hivyo
kutakuwa na BVR Kits kwa ajili ya kufanya marekebisho husika. Kwa hiyo, Mpiga Kura aliyehakiki taarifa zake
kwa kutumia njia yoyote kati ya hizo tatu zilizotajwa na kuhitaji kurekebisha taarifa zake, basi
atakwenda kwenye kituo kilichoteuliwa kwa ajili ya zoezi hilo,"alisema Kaijage.
Kwa mara nyingine
,Mwenyekiti huyo wa Tume aliwaeleza viongozi hao wa vyama jinsi Tume kuhusu
ukamilishwaji wa maandalizi kwa ajili ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili.
Alisema kwa mujibu wa
Kifungu cha 15 (5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Kifungu cha 21(5) cha
Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Tume inapaswa kuboresha Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya
Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuatia.
Aliwataja watakaohusika katika uboreshaji wa
awamu hii,kuwa ni; Wapiga Kura wapya ambao
ni raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18 au watatimiza umri huo
siku ya Uchaguzi Mkuu,waliohama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo
mengine ya kiuchaguzi, na wale ambao
kadi zao zimeharibika au kupotea.
Zoezi pia litahusisha kuwaondoa kwenye
Daftari, Wapiga Kura waliofariki na wengine waliopoteza sifa kwa mujibu wa
sheria.
Vile vile, awamu hii
itawahusu Wapiga Kura ambao hawakupata fursa kujiandikisha katika Awamu ya
Kwanza, yaani Wapiga Kura wapya au wale waliotaka kurekebisha taarifa zao.
Uboreshaji wa Daftari Awamu ya Pili ambao utaenda sambamba na
Uwekaji wazi wa Daftari la Awali utafanyika
katika “routes” tatu. Route ya
kwanza inatarajiwa kuanza tarehe 17
Aprili, 2020.
Katika Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya pili, vituo vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni kwa muda wa
siku nne (4) mfululizo.
WAPIGA KURA KUHAKIKI BURE
TAARIFA ZAO KWA KUTUMIA SIMU,TOVUTI

No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇