LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 29, 2020

MUATHIRIKA WA CORONA AWAITA MAPACHA WAKE 'CORONA' NA 'VIRUS'


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

ANNAMARIA Jose Raphael Gonzales (34) raia wa Mexico ambaye pia alikumbwa na virusi vya Corona (Covid -19) amejifungua mapacha na kuwaita Corona na Virus mtandao wa World News, Daily report umeripoti.

Imeelezwa kuwa Annamaria alikuwa akipatiwa matibabu  katika hospitali ya La Villa mjini Mexico na kujifungua mapacha hao wenye afya tele ambapo mtoto wa kike amepewa jina la Corona Jose Miguel Gonzales na kaka yake ameitwa Virus Jose  Miguel Gonzales.

Annamaria ameeleza kuwa;
"Sikuwa na jina nililopanga kuwaita, mmoja wa madaktari alishauri niwaite Corona na Virus kwa kuwa niliathirika na virusi hivyo, nikaona na wazo zuri" ameeleza.

Daktari Eduardo Castillas kutoka hospitali hiyo alivieleza vyombo vya habari kuwa alipendekeza majina hayo kwa utani tuu, ila wanashukuru mama na watoto hao wanaendelea vizuri.

"Nilimwambia awaite Corona na Virus kama utani lakini akamakinikia" ameeleza Dkt. Eduardo huku akicheka.

Annamaria alitarajia kwenda kujifungua nchini Marekani wiki ijayo lakini hakufanikiwa kuvuka mpaka.

Mwaka 2017 mwanamke mmoja kutoka Mexico alimpa mwanaye jina la Malaria baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na vimelea hivyo, na mwaka 2018 mwanamke mwingine alimpa binti yake jina la Gonorrea baada ya kukumbwa na magonjwa ya zinaa kwa vipindi mbalimbali.
 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages