LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 22, 2020

IGP SIRRO AKUTANA NA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA, AKEMEA VITENDO VYA MAUAJI

IGP Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga leo 22/01/2020 wakati alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambapo afande IGP amekutana na Makamanda wa Polisi wa mikoa mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Simiyu lengo ikiwa ni kuweka mkakati wa pamoja wa kukomesha matukio ya mauaji nchini.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amekutana na Makamanda wa Polisi wa mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuweka mikakati na mpago kazi wa pamoja katika kushughulikia matukio ya mauaji yanayojitokeza nchini ikiwa ni pamoja na kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kuwakamata na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akiwa mkoani Shinyanga IGP Sirro, amewaonya wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya imani za kishirikina vinavyopelekea mauaji yanayotokana na imani hizo na badala yake kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua wahalifu.

Aidha, IGP Sirro amemuagiza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Nchini CP Liberatus Sabas, na Makamanda wote wa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kagera, Mwanza na Simiyu kufanya operesheni ya pamoja itakayosaidia kukomesha vitendo vya mauaji nchini.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages