LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2020

MGOMBEA MTEULE WA URAIS KWA TIKETI YA CCM RAIS DK. MAGUFULI ACHUKUA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, LEO


Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akikabidhiwa mkoba wenye fomu za Uteuzi wa kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu ulipangwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Anayemkabidhi fomu hizo katika Ofisi za NEC mjini Dodoma, leo, ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage. Kushoto ni Mgombea Mwenza wa CCM Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dk. Wilson Mahera na  Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mbarouk Salim Mbarouk. Uchukuaji fomu hizo ulioanza jana, utakoma Agosti 25, 2020. 
Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza wake Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani wakati akisubiri kukabidhiwa fomu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiwa tayari kulipia fomu hizo 
Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mbarouk Salim Mbarouk akimkaribisha Dk. Magufuli na Ujumbe wake.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage akizungumza kabla ya kumkabidhi fomu Rais Dk. Magufuli ambaye naye anamsikiliza kwa makini
Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akimkabidhi mkoba wenye fomu azitie baraka Mgombea Mwenza wake Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan 
Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli na Mgombea Mwenza wake Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan wakionyesha begi lenye fomu hizo
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akionyesha mkoba wenye fomu za Rais Dk. Magufulu kuomba uteuzi wa NEC kuwania tena Urais
Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akitia saini kwenye kitabu cha wageni alipowasili ofisi za NEC kuchukua fomu hizo
Mgombea Mwenza wa Mgombea Urais wa CCM, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu alipowasili ofisi za NEC
Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akiiondoka Ofisi za NEC baada ya kuchukua fomu hizo
"Mambo Poa tuuu" Mgombea Mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli akionesha kusema hivyo wakati alipokuwa akiwasalimia wananchi waliokuwa nje alipokuwa akitoka baada ya kuchukua fomu

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages