LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 4, 2020

MKUU WA TAKWIMU WA BEI ATOA TAKWIMU ZA BEI.


Mkuu wa Takwimu za Bei katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Abdulrahman Msham akitoa Takwimu za Bei ambapo imeonekana kushuka kutoka Silimia 6.2 kwa Mwezi uliomalizikia February 2020 hadi asilimia 5.0 Mach 2020 hafla iliofanyika ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  ambapo imeonekana kushuka kutoka Silimia 6.2 kwa Mwezi uliomalizikia February 2020 hadi asilimia 5.0 Mach 2020 hafla iliofanyika ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.


Na Mwashungi Tahir 3-4-2020

Imeelezwa kwamba mfumko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 0.7 kwa mwezi wa Machi 2020 ukilinganisha na asilimia 0.8 katika mwezi February 2020.

Hayo ameyasema Mkuu wa Takwimu wa Serikali wa mfumko wa bei Khamis Abdul-rahmani Msham huko katika Ofisi za Mtakwimu Mkuu Wa Serikali Mazizini wakati akiwasilisha takwimu za bei kwa vyombo vya habari .

Amesema miongoni mwa bidhaa zilizoshuka ni pamoja na vyakula ikiwemo mchele na ndizi mbichi, vinywaji visivyo kilevi, pamoja na mafuta ya taa, Petrol na Diesel.

Nae Afisa uchumi wa Masoko ZURA Omar Ali Yussuf ameeleza kuwa bei za mafuta zinatarajiwa kushuka zaidi kutokana na hali iliyopo .

Aidha amefahamisha kuwa mafuta ya ndege yameshuka kwa kipindi hiki na uzalishaji wake umekuwa mkubwa katika soko la dunia kutokana na hali iliopo ya ugonjwa corona na kusitishwa kwa safari hivyo usafiri wa ndege umepungua.

Kwa upande wake Dkt Deogratius Philip Macha msaidizi Idara ya Uchumi kutoka Benki ya Tanzania BOT amewataka wananchi kuondoa hofu na wasiwasi wa upungufu wa chakula kwani chakula kipo cha kutosha .

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages