LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2019

NUKUU ZA KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI NDG. HUMPHREY POLEPOLE AKIHOJIWA NA RADIO GG FM- TABORA

<<KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI NDG. HUMPHREY POLEPOLE

1. "Ndg. Magufuli ana maono yake makubwa na Kila awamu huwa ina mtindo wake, kila awamu huwa ina matarajio yake na kila awamu huwa ina maono yake, lazima tukubaliane na ukweli huu" Ndg. Polepole

2. "Mtu yoyote atakayefanya kazi kwa kutuchelewesha, hatutasita, kuielekeza Serikali imchukulie hatua hadi hali ya utumishi wa umma itakapokaa sawa". Ndg. Polepole

3. "Kuna barabara ya Manyoni hadi hapa Tabora kuna kilometa 257 na zimebaki kama 80 hivi kumaliziwa kujengwa,  mkandarasi anafanyakazi, akifanya vibaya hatuacha kuelekeza Serikali imtumbue mara moja". Ndg. Polepole

4. "Wabunge wa vyama vyote wanaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo yao, sasa itakuwa ajabu Mbunge wa CCM wa hapa Tabora Mjini aende akafanye mkutano Moshi Mjini, tutamuuliza hapa Tabora Mjini amemaliza kazi zake". Ndg. Polepole

5. "Wenzetu wa upinzani wanafanya Mikutano nchi nzima, wakitoka kwenye mikutano wanasema wamezuiwa kufanya mikutano hizo ni mbinu chafu, siasa chafu na uchonganishi kwa wananchi". Ndg. Polepole

6. "Vyama vingine havikui sio kwa sababu ya kukosa mikutano ya hadhara ni kwa sababu vina utapiamlo wa kutofuata Katiba, Kanuni na Utaratibu ndani yao, vina umimi, ukanda na ukabila na kipo Chama kimeshindwa hata kujenga Ofisi ya mgongo wa tembo ya Makao Makuu hadi leo wamepanga". Ndg. Polepole

7. "Uongozi ni kazi ya kujitolea, uongozi ni dhamana na watu wanao uendea uongozi ndani ya Chama chetu lazima wawe na kazi nyingine ya kuwaingizia kipato". Ndg. Polepole

8. "Hivi tunavyozungumza wapo wadau na wataalamu wanazunguka kufuatilia zao hili la Tumbaku na kuona namna gani zao hili litaboreshwa vizuri zaidi, wananchi wawe na matumaini na Serikali yetu". Ndg. Polepole

9. "Sio Tshs. Milion 50 za kila kijiji tu, zipo fedha nyingi sana zinazotolewa na Serikali kwa wananchi wa kaya maskini na wanalipwa mishahara na zipo zaidi ya Tshs. Bilion 50 zinazotolewa bila riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu. Ni muhimu wananchi wafahamu haya, wafuatilie na kuchukua fursa hizi". Ndg. Polepole

Imetolewa na:
*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI*

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages