LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 19, 2019

RUGE MUTAHABA APACHIKWA JINA LA 'RUGE THE FIGHTER AFRIKA KUSINI'



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba amesema alipata nafasi ya kwenda Afrika Kusini kumuona Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV ambapo ameeleza Madaktari wanaomtibu Ruge wamempa jina la mpambanaji kutokana na namna anavyoumwa.

"Mimi nilipata nafasi ya kwenda South Afrika, nikaamua nikawaone madaktari wake, wamempa
jina wanamuita 'RUGE THE FIGHTER," amesema Waziri Makamba.

Katika hatua nyingine, amesema Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015, hakuhusika katika mchakato wa utungwaji kwa sababu alikuwa Naibu Waziri Mawasiliano, na mchakato ulihusisha wataalamu wa wizara, makatibu wakuu, mawaziri, na yeye hakuwa miongoni mwa makundi hayo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages