LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 11, 2019

WATOTO WALIOUNGANA WAAGA DUNIA YEMEN

Watoto pacha wa kiume walioungana wamefariki dunia nchini Yemen kutokana na mzingiro wa kila upande wa Saudi Arabia na waitifaki wake dhidi ya nchi hiyo maskini.
Wizara ya Afya ya Yemen imethibitisha habari ya kufariki dunia watoto hao pacha walioungana, kwa jina Abd al-Khaleq na Abd al-Rahim waliokuwa na umri wa wiki mbili tu.
Madaktari waliokuwa wakiwatibu watoto hao katika mji mkuu Sana'a walikuwa wamesisitizia udharura wa kupewa matibabu ya dharura watoto hao nje ya nchi, lakini hilo likashindikana kutokana na mzingiro wa Saudia dhidi ya nchi hiyo. 
Awali Saudia ilikuwa imedai kuwa ingeliwapokea pacha hao na kuwatibu katika hospitali ya nchi hiyo. Hata hivyo watoto hao ambao walikuwa wana figo moja, miguu miwili huku kila mmoja akiwa na moyo na mapafu yake wamethibitishwa kupoteza maisha usiku wa kuamkia jana Jumapili mjini Sana'a.

Watoto ndio wahanga wakuu wa hujuma mtawalia za Saudia dhidi ya Yemen

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Yemen imesema vifo vya watoto hao pacha ni taswira ya hali mbaya ya kiafya na kibinadamu inayoshuhudiwa hivi sasa nchini Yemen. 
Kwa mujibu wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF), watoto 6,700 wa Yemen wameuawa au kujeruhiwa tangu Saudi Arabia ilipoanzisha hujuma yake ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo masikini jirani yake, mnamo Machi mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages