LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 19, 2019

RAIS WA NIGERIA AWATAKA POLISI NA WANAJESHI KUTOONYESHA HURUMA KWA WEZI WA KURA


Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewaamuru polisi na wanajeshi nchini humo wasionyeshe huruma mbele ya wezi wa kura kipindi hiki wakati maandalizi yakiendelea kwa ajili ya uchaguzi huo ulioahirishwa.

uchaguzi Mkuu nchini Nigeria unatarajiwa  utafanyika Jumapili ijayo February 23, 2019, mara baada ya Tume huru ya uchaguzi nchini humo (INEC) kuhahirisha hapo February 16 mwaka huu.

INEC walitangaza kuhairishwa kwa uchaguzi huo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura.

Hata hivyo vyombo vya habari vya ndani nchini Nigeria viliripoti kuwa vifaa vya kupigia kura vilikuwa bado havijawasili katika maeneo yote nchini humo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages