LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 20, 2019

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO SABA KWA MPIGO


Mwanamke nchini Iraqi, amejifungua watoto saba kwa mpigo, hali inayoelezwa kuwa ni miongoni mwa miujiza iliyowahi kutokea duniani.

Mwanamke huyo aliyejifungua salama kupitia njia ya kawaida, anasemekana kuwa katika hali nzuri kiafya na watoto wake pia wapo katika hali nzuri.

Kulingana na ripoti ya Daily Mail, mwanamke huyo aliyejifungulia katika mkoa wa Diyali ni wa kwanza kujifungua idadi hiyo ya watoto nchini humo.

 Msemaji wa hospitali alimojifungulia mama huyo alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa, aliwasili katika hospitali hiyo na kujifungua watoto sita wa kike na mmoja wa kiume. 

Baba wa watoto hao Youssed Fadl, alisema yeye na mke wake hawakutarajia idadi hiyo ya watoto na sasa wana watoto kumi wa kulea, wakiwamo wa mbeleni.

 Pia Fadl alisema mke wake hakuwa na ufahamu angeweza kupata watoto zaidi ya mmoja kabla ya kuupata ujauzito huo. © Malunde Blog

1 comment:

  1. I've been browsing online greater than 3 hours today, but I
    by no means found any interesting article like yours.
    It's pretty worth sufficient for me. In my view, if all site
    owners and bloggers made good content material as you did, the web will
    be much more helpful than ever before.

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages