BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, January 12, 2019

BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI, ARUMERU LATEKETEA KWA MOTO

NA K-VIS BLOG, ARUMERU
BWENI la wavulana, shule ya sekondari Mlangarini iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru, limewaka moto mapema leo Januari 12, 2019.
Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Mhe. Jerry Muro aliyoitoa leo, imesema, bweni la shule hiyo mali ya serikali liliungua majira ya saa 1:02 asubuhi.
“Moto ulianza majira ya alfajiri na kuteketeza chumba kimoja kati ya vyumba kumi na nne vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 Hakuna majeruhi wala vifo,” taarifa ya DC Muro ilisema.
Hata hivyo taarifa hiyo ilisema, kuna uharibifu wa mali ikiwemo kuungua kwa  vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6), masanduku ya kuhifadhia nguo na madaftari.
“Kutokana na changamoto hiyo nililazimika kufika kwenye eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11).” Alisema Mhe. Mkuu wa wilaya Jerry Muro


No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages