LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 12, 2018

MAGAIDI WA ADF WAENDELEWA MAUAJI KONGO DR KUELEKEA UCHAGUZI

Watu 10 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ofisa mkuu wa serikali katika eneo hilo, Donat Kibwana ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, raia hao waliuawa katika mashambulizi ya ADF usiku wa kuamkia jana katika mji wa Oicha, nje kidogo ya mji wa Beni, katika eneo la Kivu Kaskazini.
Msemaji wa Jeshi la Kongo DR, Kapteni Mak Hazukay amethibitisha kutokea mauaji hayo na kuongeza kuwa, magaidi hao pia wameiba idadi kubwa ya mifugo ya wakazi wa mji huo.
Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya wapiganaji hao wa ADF wa Uganda kufanya mashambulizi mengine katika eneo la Mangolikene na Paida, katika mkoa huo wa Kivu Kaskazini na kuua raia 17.
Askari wa serikali eneo la Kivu
Kadhalika wiki iliyopita watu wengine 18 waliuawa katika mapigano kati ya jeshi na waasi watiifu kwa Jenerali muasi wa zamani wa jeshi William Amuri Yakutumba, katika eneo la Fizi katika mkoa tajiri kwa madini wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mauaji na mashambulizi hayo yanajiri katika hali ambayo, kampeni za uchaguzi zinaendelea kushika kasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu nchini humo, Desemba 23. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages