LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2018

MZEE ALI HASSANI MWINYI AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ALLY KAKURWA NA APONGEZA NIDHAMU ILIYOPO YA SERIKALI NA CHAMA

Disemba 9,  2018
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ally Hassan Mwinyi   amekutana na kuwa na mazungumzo na Ndugu Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mzee Mwinyi kwa Upendo mkubwa na   umahususi na kwa kupitia kwa Ndugu Bashiru amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri za uimarishaji wa Miundo mbinu ya kisasa na  elimu imeboreshwa kuanzia ngazi ya msingi hadi Elimu ya juu na zuri zaidi kuondoa  ada kwa wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne,  ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitatu.

Katika Mazungumzo hayo Mzee  Mwinyi   amemsihi Dr.Bashiru Ally kwamba CCM iendelee kuisimamia Serikali na kuimarisha nidhamu, kwani Elimu isiyo na nidhamu inaweza kusabisha fujo kwa watoto wetu, watumishi, watu wazima na umma kwa ujumla hii itasaidia  kuimarisha na kujenga Taifa imara na la watu wenye nidhamu ya kuheshimu kanuni,taratibu na sheria za nchi ili kuendelea kuchapa kazi sambamba na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu yenye dhamira ya kuleta Maendeleo.

Aidha Mzee Ally Hassan Mwinyi Ameipongeza serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi kwa Kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania, kwani kiswahili ndiyo lugha ya pekee  inayo tambulisha Nchi yetu

Akipokea pongezi hizo Ndugu Bashiru Ally amemshukuru Mzee Ally Hassani Mwinyi kwa kuendelea kutoa Mchango wake mkubwa katika kuimarisha Muungano na kukuza lugha ya kiswahili kwani kiswahili ni lugha yetu ya Taifa na  Ndugu Bashiru Ally amesisitiza  kuwa Mzee Mwinyi  ni Rais aliyeweza kuwa na Mchango mkubwa katika serikali zote mbili na ameendelea kutukumbusha, kutushauri na kutuombea kila anapopata nafasi. 

Ndugu Bashiru amemjulisha mzee Mwinyi  kwamba tarehe 17 na 18 Desemba kutafanyika vikao vya Uongozi vya Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwaka 2015 - 2020.

Huu ni muendelezo wa ziara na mazungumzo ya Ndugu Bashiru Ally na viongozi, makada na wanachama wa CCM ili kupokea ushauri, kubadilishana nao uelewa, mipango, mikakati na taarifa za ujenzi wa Chama.

Imetolew na 
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages