LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 18, 2018

ETHIOPIA YAWAACHAIA HURU WATU 1, 174 WALIOHUSISHWA NA MACHAFUKO YA ADDIS ABABA

Serikali ya Ethiopia imetangaza habari ya kuachiwa huru mamia ya watu waliokamatwa wakati wa ghasia zilizoshuhudiwa mwezi uliopita wa Septemba katika mji mkuu, Addis Ababa.
Mkuu wa Polisi nchini humo, Jemal Zeinu amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, miongoni mwa vijana 1,200 waliokamatwa wakati wa machafuko hayo, 1,174 wameachiwa huru huku 83 wakitazamiwa kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhusika na ghasia hizo.
Polisi ya Ethiopia imesema watu 23 waliuawa katika machafuko hayo, huku mamia ya wengine wakitiwa mbaroni wakihusishwa na machafuko hayo ambayo yalilaaniwa vikali na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa nchi ambaye tangu aingie madarakani amefanya mabadiliko makubwa hususan ya kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na jirani yake Eritrea.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International sanjari na kupongeza hatua hiyo, lakini limesema serikali ya Addis Ababa inapaswa kujiepusha na kamatakamata kinyume cha sheria.
Maafisa wa polisi wakishika doria mjini Addis Ababa
Ghasia hizo zilizofanyika kati ya Septemba 12 na 17, ziliibuka baada ya wafuasi wa kundi la zamani la waasi la Harakati ya Ukombozi wa Oromo (OLF) ambao wengi wao wanatoka kabila la Oromo, kuingia mjini Addis Ababa wakipeperusha bendera ya OLF na kupambana na wakazi wa mji huo.
Waoromo ambao ni takribani asilimia 33 ya watu wote milioni 100 nchini Ethiopia wanaitazama OLF na bendera yake kuwa ni nembo ya mapambano ya miongo kadhaa ya kupinga ubaguzi wa watawala wasio Waoromo nchini humo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages