LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 18, 2018

DIWANI BUJUGO WA KATA YA MAGOMENI AFARIKI DUNIA LEO

Diwani wa Kata ya Magomeni, jijini Dar es Salaam, Julian Rushaigo Bujugo (pichani) amefariki dunia

Taarifa zilizotangazwa zimesema Bujugo, amefariki dunia saa 6.45 usiku wa kuamkia leo tarehe 18. 10. 2018 katika Hospitali ya Massana Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam alikopelekwa baada ya kuugua ghafla.

Taarifa zinasema hadi jana saa 9.00 mchana, Oktoba 17, 2018 Bujugo aliachana na Madiwani Wenzake kwenye ofisi za Manispaa  ya Kinondoni akiwa mzima wa Afya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Bujugo wakati wote alikuwa akisumbuliwa na Sukari na mwili wake kwa sasa umehifadhiwa katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages