LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2018

DK. BASHIRU AWASILI MKOANI LINDI AKIENDELEA NA ZIARA MIKOA YA KUSINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Bashiru Ally  leo Tarehe 23 Septemba amewasili Mkoani Lindi akitokea Mkoani Mtwara ambapo  amepokelewa na Viongozi na wanachama wa CCM katika eneo la Mnazi Mmoja  katika Manispaa ya Lindi.

Akihutubia viongozi na wanachama hao waliojitokeza kumpokea , Ndg.Katibu Mkuu amewataka Watanzania wote kushikamana pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kufuatia ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere   iliyotokea Wilayani Ukerewe Mkoani   Mwanza.

" Kupitia wana Lindi  wa hapa ,nawaomba tujumuike pamoja  katika maombelezo ya kuwafariji ndugu zetu na jamaa waliopoteza ndugu zao, jamaa na marafiki katika Ajali ya Mv Nyerere. Marehemu wote waliotangulia mbele za haki tuwaombee makao mema ya Milele" Amesema Katibu Mkuu wa CCM.

Ziara hiyo Imemfikisha hadi Wilaya ya Nachingwea ambapo amekagua Miradi  mbalimbali ya CCM ikiwemo Mradi wa ujenzi wa vibanda 52 vya Biashara  chini ya usimamizi wa Kamati ya siasa (CCM) Wilaya ya Nachingwea.
Mradi huo unatarajia  Kuongeza vyanzo vya  Mapato vya Chama Cha Mapinduzi na  unatarajiwa kukamilika mwezi Octoba 2018, na kugharimu kiasi cha. Tsh. 156,000,000/=

Ndg. Bashiru atakua na ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo ya kukagua Uhai wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na kufungua kampeni katika Jimbo la Liwale mnamo Tarehe 25 Septemba.

Huu ni mwendelezo wa kukagua na kuimarisha Uhai wa Chama Cha Mapinduzi  katika  Mikoa   ya Kusini kwa ngazi zote za Mikoa, Wilaya, Kata, Matawi na Mashina.

Imetolewa na:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages