LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2018

WAZIRI MKUU: TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA KUWAIT


Ameyasema hayo Ijumaa, Agosti 3, 2018 wakati alipokutana na Balozi wa Kuwait nchini, Balozi Jasem Al Najemkatikamakazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Balozi Al Najem ambaye anamaliza muda wake, amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga na kwamba leo anatarajia kuondoka nchini na kurejea Kuwait.

Waziri Mkuu amemshukuru balozi huyo kwa ushirikiano alioutoa Tanzania katika kipindi chote cha uwakilishi wake na kwamba nchi hizo zinatarajia kuanza ushirikiano katika usafiri wa anga.

Amesema Kuwait ni moja kati ya nchi rafiki, ambayo imeshirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa shughuli za maendeleo kupitia Balozi Najem, hivyo wataendelea kumkumbuka.

“Balozi Najem amejitoa sana katika kuwasaidia Watanzania hususan kwenye miradi ya huduma za jamii kwa kupeleka maji mashuleni, vituo vya afya, zahanati na hospitalini,”.

“Pia Ubalozi wa Kuwait umesaidia kuleta vifaa tiba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na madaktari katika baadhi ya hospitali nchini. Ushirikiano huu umeleta tija sana,” amesema.

Waziri Mkuu amesema mbali na miradi hiyo ya huduma za jamii, pia balozi huyo ameshiriki kuendeleza Sekta ya utalii nchini kwa kuleta watalii wengi kutoka nchini Kuwait kuja Tanzania.

Waziri Mkuu meongeza kuwa Balozi Al Najem ameshiriki kikamilifu katika kuratibu shugughuli zote za maendeleo kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuunganisha sekta binafsi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amemuhakikisha balozi huyo kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Kuwait na kwamba ipo tayari kumpokea mwakilishi mwingine.

Kwa upande wake, Balozi Al Najem ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompa katika kipindi chote alichokuwa akiiwakisha Serikali ya Kuwait nchini.

Amesema tangu alipowasili nchini amekuwa akipewa ushirikiano mkubwa na viongozi wote wa Serikali jambo lililomrahisishia utekelezaji wa majukumu yake nchini.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages