Thursday, August 2, 2018

WAMAREKANI WEUSI WAANDAMANA KULAANI MAUAJI MAPYA YA POLISI DHIDI YA VIJANA WAO

Wamarekani weusi wa mji wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota nchini Marekani, wamefanya maandamano makubwa kulaani mauaji ya polisi dhidi ya kijana mmoja mwenye asili ya Kiafrika katika mji huo.
Maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wanaharakati mbalimbali wa haki za binaadamu na watu wa familia ya kijana mmoja mwenye asili ya Kiafrika aliyeuawa hivi karibuni kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi wa mji huo, yalipelekea kukwama harakati za magari. Katika maandamano hayo, washiriki walitaka kutiwa mbaroni polisi wote waliohusika na tukio la kumfyatulia risasi kumlenga kijana huyo aliyetambuliwa kwa jina la Thurman Blevins.
Thurman Blevins, kijana aliyeuawa
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Thurman Blevins aliuawa tarehe 23 Juni mwaka huu, wakati polisi walipokuwa wanamkimbiza. Polisi wanadai kwamba, walimmiminia risasi kijana huyo baada ya yeye kuanza kuwarushia risasi polisi, ingawa video iliyoonyeshwa na polisi haijathibitisha iwapo Blevins alikuwa na silaha wala kufyatua risasi. Habari mbalimbali zimeelezea ongezeko la vitendo vya ukatili na jinai dhidi ya jamii za walio wachache na Wamarekani weusi ndani ya nchi hiyo. Aidha takwimu zinaonyesha kwamba, wahanga wengi wa mashambulizi ya kufyatuliwa risasi nchini Marekani ni Wamarekani wenye asili ya Kiafrika. 
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.