LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 2, 2018

UNICEF: SAUDIA IACHE KUSHAMBULIA MIUNDOMBINU YA YEMEN

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa Unicef, umeutaka utawala wa Aal-Saud, ukomeshe mashambulizi yake dhidi ya miundombinu ya Yemen.
UNICEF, imetoa taarifa hiyo Jumatano ya jana ambapo pamoja na mambo mengine imeutaka muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudia, ukomeshe mashambulizi yake dhidi ya miundombinu ya msingi ya Wayemen, hususan kwenye vyanzo vya maji vya nchi hiyo. Kabla ya hapo pia Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa Unicef ulitaka kupatikana njia ya ufumbuzi wa kisiasa na kutolewa fursa ya kurejesha amani nchini Yemen. Hii ni katika hali ambayo, muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia, umekuwa ukifanya mashambulizi makali dhidi ya vyanzo vya maji na miundombinu ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Jinai zinazofanywa na Saudia nchini Yemen
Jinai mpya kabisa za ndege za muungano huo vamizi nchini Yemen, ni kushambulia ghala moja la kuhifadhia bidhaa za mahitaji ya msingi ya wakimbizi wa Yemen mali ya Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF). Hujuma hizo za kila siku za Saudia dhidi ya Yemen zilizoanza tangu mwezi Machi 2015, hadi sasa zimepelekea mauaji ya zaidi ya watu elfu 14 na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages