BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, August 5, 2018

RAIS MAGUFULI AWAOMBA WATANZANIA KUMUOMBEA WAZIRI DKT. KIGWANGALA NAFUU YA HARAKA BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA HUKO MANYARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara mara baada ya kuwasili kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la kubeba wagonjwa kwa tayari kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu Zaidi mara baada ya kuletwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo alasiri Agosti 4, 2018. Dkt. Kigwangala akiwa na wasaidizi wake, wakitumia gari aina ya Land Cruiser V8 alipata jail baada ya gari lake kujaribu kumkwepa Twiga eneo la Magugu mkoani Manyara na kupelekea gari hilo kupinduka, na kusababisha kifo cha afisa habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Hamza Temba. Rais amewataka Watanzania kumuombea Dkt. Kigwangala na majeruhi wengine wa ajali hiyo na kumjuelezea kwamba ni waziri mchapakazi na alikuwa katika safari ya kikazi. "Migwangala ni waziri mchapakazi ninyi wenyewe mnaona kila siku yuko huko na kule na kwakweli viongozi wote wa Wkizara akiwemo naibu wake, wanafanya kazi kubwa, lililobaki tuwaombee kwa Mwenyezimungu wapone haraka na warejee katika kazi zao." Aliasa Mhe. Rais wakati akizungumza muda mfupi baada ya kuongoza maafisa wa serikali kumpokea Dkt. Kigwangala kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akitokea jijini Arusha alikopelekwa kwa matibabu ya awali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani Manyara.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika  ajali ya gari mkoani Manyara.


  Ndege maalumu iliyombeba Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  kutokea mkoani Arusha majira ya jioni.(PICHA NA IKULU)


Hoili ndilo gari lililomchukua Dkt. Kigwangala kama linavyoonekana baada ya kupinduka

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages