LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 5, 2018

RAIS MADURO WA VENEZUELA ANUSURIKA JARIBIO LA MAUAJI, AITUHUMU MAREKANI, COLOMBIA

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amenusurika jaribio la mauaji lililofanywa na kitu kinachoaminika kuwa ni ndege isiyo na rubani (drone).
Jaribio hilo limefanyika wakati Rais wa Venezuela alipokuwa akihutubia katika kambi ya jeshi usiku wa kuamkia leo mjini Caracas.
Baada ya kunusurika jaribio hilo, Maduro amesema kuwa Marekani na Colombia ndizo zilizofanya jaribio la kutaka kumuua. Amesema "Ilikuwa hujuma ya kutaka kuniua na Marekani pamoja na Colombia zimehusika."
Amesema kuwa vyombo husika vimeanza uchunguzi mara moja na kwamba watu kadhaa wametiwa nguvuni kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.
Rais wa Venezuela amesisitiza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu waliopanga jaribio la kutaka kumuua wanaishi Florida nchini Marekani na ameitaka serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kusaidia uchunguzi huo. 
Maduro na maafisa wa serikali na jeshi la Venezuela katika fadhaa baada ya kushambuliwa.
Wakati huo huo Waziri wa Habari wa Venezuela, Jorge Rodriguez amesema kuwa walinzi saba wa Rais wa nchi hiyo wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.
Awali picha za televisheni zilimuonesha Maduro akihutumia gwaride la jeshi kabla ya kuhujumiwa na ndege isiyo na rubani na baadaye kidogo walionekana askari wakikimbia huku na kule katika jaribio la kuokoa maisha yao.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages