LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 9, 2018

RAIS DK.. MAGUFULI AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MZEE MAJUTO KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM, LEO, ATOKWAMACHOZI YA HUZUNI


Rais Dk. John Magufuli akijifuta machozi alipokuwa akiaga mwili wa aliyekuwa msanii nguli wa vichekesho hapa nchini na nje ya nchi Mzee Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa nguli huyo wa uchekeshaji iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Agosti 9, 2018.

Rais Magufuli alifika Karimjee na kuungana na maimia ya waombolezaji wakiwemo viongozi mbalimbali pamoja na Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete katika kuaga mwili wa nguli huyo aliyefariki dunia jana Jumatano, saa 2 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili alipokuwa akitibiwa.

Mwili wa Mzee Majuto umesafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga ambako atazikwa kesho Ijumaa, Agosti 10, 2018 mchana.
Rais Dk Magufuli akimfariji mmoja wa ndgu wa Mzee Majuto
 Rais Dk magufuli akitoa heshima zake za mwisho
 Rais mstaafu Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho
 Rais dk Maguli akiwa na Rais mstaafu Dk, jakaya Kikwete wakati wa dua ya kuombea marehemu Mzee Majuto wakati wa kuaga mwili

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages