BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 1, 2018

NDEGE YAANGUKA MUDA MFUPI BAADA YA KURUKA, ABIRIA WOTE 103 WAMENUSURIKA

NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
ABIRIA wote 103 na wahudumu wa ndege ya Aeroméxico aina ya Embraer 190wamenusurika katika ajali ya ndege iliyotokea leo Agosti 1, 2018 kwenye mji wa Durango nchini Mexico.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kimataifa vikimnukuu Gavana wa mji huo Jose Rossa Aispuro, alisema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali aliosababisha ndege  bawa moja la ndege hiyo kukita ardhini na injini zote mbili kuchomoka.
Watu 97 kati ya hao 103, ndio wanaripotiwa kuwa wamejeruhiwa ambapo abiria wengi waliweza wao wenyewe kutoka kwenye ndege hiyo muda mfupi kabla ya kulipuka na kushika moto.
Afisa Mtendaji Mkuu wa ndege hiyo, Andres Conesa amesema rubani wa ndege hiyo amepata majeraha
“Rubani wa ndege anafanyiwa upasuaji, na tunachojua kwa sasa majeraha hayo hayatishii maisha yake kwa” Alisema.
Hata hivyo majina na utaifa wa abiria hao walionusurika bado havijafahamika kwa sasa
Ndege hiyo ya Aeroméxico mruko ( flight) numba  AM2431 ilikuwa inaruka kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Guadalupe Victoria kuelekea mji mkuu,  Mexico City.
Afisa wa uwanja wa ndege Grupo Aeroportuario Centtro amesema hali mbaya ya hewa ndio chanzo cha ajali hiyo na kwamba, wakati ndege hiyo inaruka, ilikumbana na upopo mkali ulioilazimisha kujaribu bkutua kwa dharura lakini pawa moja lilikita ardhini na kupelekea injini kuchomoka.

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages