LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2018

MZEE MAJUTO ALAZWA CHUMA CHA UANGALIZI MUHIMBILI

Msanii maarufu wa maigizo Amri Athuman maarufu ‘King Majuto’ amelazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa MNH Aminiel Aligaesha amesema Majuto aliletwa hospitalini hapo Jumanne wiki hii saa 12 jioni.

“Ni kweli yupo chumba cha wagonjwa mahututi, tunaye hapa,” amesema.

Ofisa Habari wa Chama cha Waigizaji Kinondoni Masoud Kaftany naye amethibitisha taarifa hizo.

“Tayari madaktari wameanza kufanya vipimo ili kubaini ugonjwa unaomsumbua,” amesema.

Hii ni mara ya pili kwa Mzee Majuto kulazwa MNH, mara ya kwanza alilazwa kabla ya kwenda India kwa upasuaji wa tezi dume.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages