Monday, August 6, 2018

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA MTO MBEZI NA MBWENI,AZUNGUMZA NA BAADHI YA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akizungumza na baadhi ya Vijana wanaochimba mchanga ndani ya mto Mbezi kwa madai ya kuondoa mchanga ndani ya mto huo ili kuongeza kina chake kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo kuona namna shughuli za uondoaji mchanga katika eneo unavyoendelea ikiwemo na kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya mto huo kuhusiana na shughuli hiyo. 
Shughuli za uondoaji Mchanga ndani ya Mto Mbezi ukiendelea
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kampuni Benson Construction Ltd,Adam Kapama mapema leo,kuhusu shughuli nzima ya kuondoa mchanga ndani ya mto Mbezi ili kuongeza kina kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko, ikiwemo pia kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya maeneo hayo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kati) akimsikiliza mmoja wa Wakazi waishio kando kando ya Mto Mbezi,kuhusiana na shughuli nzima inayoendelea ya kuondoa mchanga ndani ya mto Mbezi ili kuongeza kina kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko, ikiwemo pia kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya maeneo hayo. 
Shughuli za uondoaji Mchanga ndani ya Mto Mbezi ukiendelea 
Mmoja wa Wakazi waishio Mbweni Teta,Emanuel Maingu akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh.Daniel Chongolo (pichani kulia) namna wanavyoathiriwa na tatizo la maji kutuama kwa mda mrefu wakati wa mvua zinaponyesha. Mh Chongolo ametembelea maeneo ya Mto Mbezi pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kushoto) akimsikiliza Mmoja wa wakazi wa Mbweni Teta,Emanuel Maingu namna walivyoathirika na mafuriko ikiwemo na kutuama kwa maji muda mrefu wakati wa Mvua zinaponyesha katika maeneo yao.Mh Chongolo ametembelea maeneo ya Mto Mbezi pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.