LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 7, 2018

KIKWETE ATAKA TEKNOLOJIA MPYA YA KILIMO IWAFIKIE WANANCHI

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ametaka teknolojia mpya ya kilimo, ufugaji na uvuvi inayoonyeshwa wakati wa maonyesho ya wakulima na wafugaji maarufu kama Nanenane, iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika umasikini.

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea vipando na mabanda katika maonesho hayo Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.

Alisema pamoja na wataalamu wa sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi kuvumbua teknolojia mpya katika sekta hiyo, bado haiwafikii wananchi wa vijijini.

Hivyo amewataka watalaamu hao pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua, elimu hiyo waipeleke kwa wananchi ili kuondoa umasikini miongoni mwao.

“Kazi kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya ubora, suala kubwa ni namna gani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu utawafikia wakulima,” alisema Kikwete.

Alisema ili kuondokana na umasikini kwa haraka, wataalamu wanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kibiashara na kuondokana na dhana ya kufanya kazi hizo kwa kujikimu peke yake.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages