Tuesday, August 7, 2018

DKT. KALEMANI AIAGIZA TANESCO KUANZA KUNUNUA VIUNGANISHI (ACCESSARIES) HAPA HAPA NCHINI IFIKAPO NOVEMBA MWAKA HUU

 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akionyeshwa kiunganishi cha nguzo za umeme na mashine nyingine kwenye kiwanda cha Auto Mech Limited cha jijini Dar es Salaa leo Agosti 6, 2018 wakati wa ziara yake ya kuangalia uwezo wa kiwanda hicho katika uzalishaji wa vifaa hivyo.
  NA MWANISHI WETU
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, ametoa miezi mitatu kama kipindi cha mpito kwa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini REA, kuanza kununua  viunganishi (Accessories), kutoka kwa wazalishaji wa hapa nchini.
Mhe. Waziri ametoa maagizo hay leo Agosti 6, 2018 wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza viunganishi vya vyuma na mashine, cha Auto Mech Limited kilichoko Tabata jijini Dar es Salaam ili kujionea uwezo wa kiwanda hicho wa kuzaisha vifaa hivyo.
“Nimekuja hapa ili kujiridhisha kama kiwanda hiki kinao uwezo wa kuzalisha viunganshi vya kutosha, na kwakweli nimejiridhisha kuwa kiwanda hiki kinao uwezo wa kuzalisha vifaa hivyo na nimetoa kipindi cha mpito cha miezi mitatu (3) ili TANESCO na REA wajiandae sasa kuagiza vifaa hapa hapa nchini.” Alisema Dkt. Kalemani.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.