Monday, July 30, 2018

WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO CHA MV. MWANZA

 Kivuko kipya cha MV. Mwanza kushoto kikiwa kimepaki katika maegesho ya Kigongo, kulia kwake ni kivuko cha MV. Misungwi ambavyo vyote kwa pamoja vina uwezo wa kubeba uzito wa tani 250, sawa na abiria 100 na magari 36 kwa wakati mmoja. Eneo la Kigongo/ Busisi sasa lina jumla ya vivuko vinne; Mv. Mwanza, Mv. Misungwi, Mv. Sengerema pamoja na Mv. Sabasaba.(PICHA NA THERESIA MWAMI – TEMESA)  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe (wa tano kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wakishangilia kukamilika kwa zoezi la kupokea kivuko kipya cha MV. MWANZA. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe (katikati) akikata utepe uliofungwa kwenye kivuko cha MV. MWANZA kuashiria kukamilika mapokezi ya kivuko hicho. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.