LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2018

WANASAYANSI WAWILI WA PALESTINA WAKUTWA WAMEAGA DUNIA HUKO ALGIERS

Wanasayansi wawili wa Kipalestina wamekutwa wameaga dunia katika nyumba moja huko Algiers mji mkuu wa Algeria. Hayo yameelezwa na ubalozi wa Palestina nchini humo.
Suliman al Farra aliyekuwa na umri wa miaka 34 na Mohammed al Bana wote kutoka eneo la Khan Younis katika Ukanda wa Ghaza jana walikutwa wameaga dunia  katika nyumba moja huko Algiers.
Kulingana na uchunguzi wa awali, imeelezwa kuwa raia hao wa Palestina huwenda wamepoteza maisha kutokana na kuvuta gesi au kwa shoti ya umeme. Hata hivyo ripoti kutoka Palestina zimesema wanasayansi hao wawili wameuawa.
Wakala mmoja wa habari katika Ukanda wa Ghaza umearifu kuwa vifo vya wanasayansi hao vilitokea siku mbili zilizopita na waligundulika wameaga dunia jana jioni baada majirani kuhisi harufu ya gesi iliyoenea katika nyumba hiyo.
Polisi ya Algeria ilikuta miili ya Waplestina hao mmoja ukiwa karibu na mlango na mwingine kitandani. Wanasayansi kadhaa wa Palestina wameuawa katika miaka ya karibuni katika maeneo tofauti duniani huku vifo vingi vikihusishwa na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad).

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages