LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 3, 2018

WAHAJIRI 63 WAHOFIWA KUFA MAJI BAADA YA BOTI YAO KUZAMA PWANI YA LIBYA

Wahajiri 63 wametoweka baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya, wakiwa katika jitihada za kuvuka bahari ya Mediterranean na kuingia barani Ulaya kutafuta maisha.
Jenerali Ayoub Kacem, msemaji wa Jeshi la Majini la Libya amesema boti hiyo imezama katika eneo la Garaboulli, mashariki mwa mji mkuu Tripoli.
Kwa mujibu wa manusura wa ajali hiyo, boti hiyo ilikuwa imebeba wahajiri 104, ambapo 41 waliokuwa wamevalia mafulana ya usalama (life jackets) wameweza kuokolewa.
Mbali na hao 41, Gadi ya Pwani ya Libya jana Jumatatu iliokoa pia wahajiri wengine 235, wakiwemo watoto wadogo 54 na wanawake 29 na kuwarejesha mjini Tripoli.


Makumi ya wahajiri katika safari hatarishi ya kuelekea Ulaya

Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya watoto wadogo watatu kuaga dunia baada ya kuzama boti katika pwani ya Libya. Watu 16 waliokolewa katika tukio hilo, huku wahajiri karibu 100 wakitoweka.
Libya ndio lango kuu linalotumiwa na wakimbizi wanaojaribu kuelekea Ulaya kwa njia ya bahari. Kwa miaka kadhaa sasa wakimbizi wengi wamekuwa wakivuka bahari ya Mediterrania wakielekea Ulaya, ingawaje maelfu miongoni mwao wamepoteza maisha kwa kuzama baharini.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages